1 Kings 14:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akaichukua hazina yote ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ya ikulu; alichukua kila kitu; pia alichukua ngao zote za dhahabu alizozitengeneza Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akachukua hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao zote za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa amezitengeneza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akazichukua hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao zote za dhahabu alizozifanya Sulemani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akaichukua hazina yote ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ya ikulu; alichukua kila kitu; pia alichukua ngao zote za dhahabu alizozitengeneza Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akachukua hazina yote ya Hekalu la BWANA na hazina yote ya jumba la kifalme. Alichukua kila kitu, pamoja na ngao zote za dhahabu Solomoni alizotengeneza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akachukua hazina za Hekalu la bwana na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao zote za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa amezitengeneza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao zote za dhahabu alizozifanya Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akaichukua hazina yote ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ya ikulu; alichukua kila kitu; pia alichukua ngao zote za dhahabu alizozitengeneza Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akavichukua vilimbiko vya Nyumbani mwa Bwana navyo vilimbiko vya nyumbani mwa mfalme, vyote pia akavichukua, nazo ngao za dhahabu, Salomo alizozitengeneza, akazichukua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao zote za dhahabu alizozifanya Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaitwaa hazina yote ya nyumba ya Yawe na ya nyumba ya kifalme. Alitwaa kila kitu; naye alitwaa ngao zote za zahabu Solomono alizozitengeneza.