1 Kings 15:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baasha, mfalme wa Israeli, aliishambulia nchi ya Yuda na kuanza kuujenga Rama ili apate kuzuia mtu yeyote asitoke wala asiingie kwa Asa, mfalme wa Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome katika mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia katika nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, Baasha mfalme wa Israeli akaondoka juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baasha, mfalme wa Israeli, aliishambulia nchi ya Yuda na kuanza kuujenga Rama ili apate kuzuia mtu yeyote asitoke wala asiingie kwa Asa, mfalme wa Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baasha mfalme wa Israeli akakwea dhidi ya Yuda na kuweka ngome Rama ili kuzuia ye yote kuingia au kutoka katika nchi ya Asa mfalme wa Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, Baasha mfalme wa Israeli akashambulia Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu yeyote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baasha, mfalme wa Israeli, aliishambulia nchi ya Yuda na kuanza kuujenga Rama ili apate kuzuia mtu yeyote asitoke wala asiingie kwa Asa, mfalme wa Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basa, mfalme wa Waisiraeli, akapanda kuijia nchi ya Yuda, akajenga Rama, asipatikane mtu anayeweza kutoka wala kuingia kwa Asa, mfalme wa Wayuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, Baasha mfalme wa Israeli akaondoka juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basha, mufalme wa Israeli, aliishambulia inchi ya Yuda na kuanza kuujenga muji wa Rama kusudi apate kuzuia mutu yeyote asitoke wala asiingie kwa Asa, mufalme wa Yuda.