1 Kings 15:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo mfalme Ben-hadadi akakubali pendekezo la mfalme Asa, akawatuma majemadari wake na majeshi yake kwenda kuishambulia miji ya Israeli. Nao wakateka Iyoni, Dani, Abel-beth-maaka, Kinerethi yote, na nchi yote ya Naftali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote, pamoja na Naftali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo mfalme Ben-hadadi akakubali pendekezo la mfalme Asa, akawatuma majemadari wake na majeshi yake kwenda kuishambulia miji ya Israeli. Nao wakateka Iyoni, Dani, Abel-beth-maaka, Kinerethi yote, na nchi yote ya Naftali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na akatuma majemadari wake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote pamoja na Naftali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote, pamoja na Naftali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo mfalme Ben-hadadi akakubali pendekezo la mfalme Asa, akawatuma majemadari wake na majeshi yake kwenda kuishambulia miji ya Israeli. Nao wakateka Iyoni, Dani, Abel-beth-maaka, Kinerethi yote, na nchi yote ya Naftali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Benihadadi akamwitikia mfalme Asa, akawatuma wakuu wa vikosi vyake, alivyokuwa navyo, kwenda kupigana na miji ya Waisiraeli, akaipiga miji ya Iyoni na Dani na Abeli-Beti-Maka na Kineroti yote, hata nchi yote ya Nafutali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo mufalme Beni-Hadadi akakubaliana na mufalme Asa, akawatuma majemadari wake na waaskari wake kwenda kuishambulia miji ya Israeli. Nao wakateka miji Iyoni, Dani, Abeli-Beti-Maka, Kineroti yote, na inchi yote ya Nafutali.