1 Kings 15:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mfalme Asa alipotoa tangazo kwa watu wote wa Yuda, bila kumwacha hata mtu mmoja, wahamishe mawe ya Rama na mbao, vifaa ambavyo Baasha alivitumia kujengea. Kisha mfalme Asa alitumia vifaa hivyo kujengea Geba, katika Benyamini na Mizpa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumwacha hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akizitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyo Benyamini na Mispa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mfalme Asa alipotoa tangazo kwa watu wote wa Yuda, bila kumwacha hata mtu mmoja, wahamishe mawe ya Rama na mbao, vifaa ambavyo Baasha alivitumia kujengea. Kisha mfalme Asa alitumia vifaa hivyo kujengea Geba, katika Benyamini na Mizpa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumbagua hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyoko Benyamini na Mispa pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumbagua hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyoko Benyamini na Mispa pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo mfalme Asa alipotoa tangazo kwa watu wote wa Yuda, bila kumwacha hata mtu mmoja, wahamishe mawe ya Rama na mbao, vifaa ambavyo Baasha alivitumia kujengea. Kisha mfalme Asa alitumia vifaa hivyo kujengea Geba, katika Benyamini na Mizpa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme Asa alipowapigia Wayuda wote mbiu kwamba: Hakuna asiyepaswa na kazi yangu. Kwa hiyo wakayachukua mawe ya huko Rama nayo miti yake, Basa aliyoitumia ya kujenga, naye mfalme Asa akaitumia ya kujenga Geba wa Benyamini na Misipa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme Asa akatoa tangazo kwa watu wote wa Yuda, bila kumwacha hata mutu mumoja, wahamishe mawe ya Rama na mbao, vifaa ambavyo Basha alivitumia kwa kujenga. Kisha mufalme Asa alitumia vifaa hivyo kwa kujenga kuta za Geba, katika inchi ya Benjamina na Misipa.