1 Kings 15:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matendo mengine yote ya Asa, ushujaa wake na miji yote aliyoijenga, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Wafalme wa Yuda. Lakini, wakati wa uzee wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Hata hivyo, katika uzee wake alishikwa na ugonjwa wa miguu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mambo yote ya Asa yaliyosalia, na nguvu zake zote, na yote aliyoyafanya, na miji aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? Lakini alipokuwa mzee alikuwa na ugonjwa wa miguu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matendo mengine yote ya Asa, ushujaa wake na miji yote aliyoijenga, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Wafalme wa Yuda. Lakini, wakati wa uzee wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda? Katika uzee wake, hata hivyo, alipata ugonjwa wa miguu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Katika uzee wake, hata hivyo, alipata ugonjwa wa miguu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mambo yote ya Asa yaliyosalia, na nguvu zake zote, na yote aliyoyafanya, na miji aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? Lakini alipokuwa mzee alikuwa na ugonjwa wa miguu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Matendo mengine yote ya Asa, ushujaa wake na miji yote aliyoijenga, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Wafalme wa Yuda. Lakini, wakati wa uzee wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo mengine yote ya Asa na matendo yake ya vitani yenye nguvu, hayo yote, aliyoyafanya, nayo miji aliyoijenga, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda? Lakini alipokuwa mzee akaugua miguu yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mambo yote ya Asa yaliyosalia, na nguvu zake zote, na yote aliyoyafanya, na miji aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? Lakini alipokuwa mzee alikuwa na ugonjwa wa miguu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Matendo mengine yote ya Asa, ushujaa wake na miji yote aliyoijenga, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Siku za Wafalme wa Yuda. Wakati wa uzee wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu.