1 Kings 15:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu alipoanza kutawala, Baasha akawaua watu wote wa jamaa ya Yeroboamu; hakuacha hai hata mtu mmoja wa jamaa ya Yeroboamu; hiyo ilikuwa sawa na yale aliyosema Mwenyezi-Mungu kwa njia ya mtumishi wake, Ahiya wa Shilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tu alipoanza kutawala, aliwaua watu wote wa nyumba ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu hata mtu mmoja akiwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa mara alipotawala, akawapiga nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu mwenye pumzi ye yote, hata alipomharibu sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa mtumishi wake Ahiya, Mshiloni;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu alipoanza kutawala, Baasha akawaua watu wote wa jamaa ya Yeroboamu; hakuacha hai hata mtu mmoja wa jamaa ya Yeroboamu; hiyo ilikuwa sawa na yale aliyosema Mwenyezi-Mungu kwa njia ya mtumishi wake, Ahiya wa Shilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tu alipoanza kutawala, aliua jamaa yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu ye yote aliyekuwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno la BWANA lililotolewa kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tu alipoanza kutawala, aliua jamaa yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu yeyote aliyekuwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno la bwana lililotolewa kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa mara alipotawala, akawapiga nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu mwenye pumzi yeyote, hata alipomharibu sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mtumishi wake Ahiya, Mshiloni;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tu alipoanza kutawala, Baasha akawaua watu wote wa jamaa ya Yeroboamu; hakuacha hai hata mtu mmoja wa jamaa ya Yeroboamu; hiyo ilikuwa sawa na yale aliyosema Mwenyezi-Mungu kwa njia ya mtumishi wake, Ahiya wa Shilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipokwisha kuwa mfalme akawaua wote waliokuwa wa mlango wa Yeroboamu, hakusaza hata mmoja aliyevuta pumzi kwao wa Yeroboamu, akawamaliza kabisa, kama Bwana alivyosema kinywani mwa mtumishi wake Ahia wa Silo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa mara alipotawala, akawapiga nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu mwenye pumzi ye yote, hata alipomharibu sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mtumishi wake Ahiya, Mshiloni;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara tu alipoanza kutawala, Basha akawaua watu wote wa jamaa ya Yeroboamu; hakuacha muzima hata mutu mumoja wa jamaa ya Yeroboamu. Hiyo ilikuwa sawa na yale Yawe aliyosema kwa njia ya mutumishi wake Ahiya wa Shilo.