1 Kings 16:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu alipoanza kutawala, Zimri aliwaua watu wote wa jamaa ya Baasha; hakumwachia hata mwanamume mmoja wa jamaa yake wala wa rafiki zake;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tu alipoanza kutawala na kukalia kiti chake cha kifalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, alipoanza kutawala, mara alipoketi juu ya kiti chake cha enzi, akawaua nyumba yote ya Baasha; hakumwachia mwanamume ye yote, wa jamaa zake, wala wa rafiki zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu alipoanza kutawala, Zimri aliwaua watu wote wa jamaa ya Baasha; hakumwachia hata mwanamume mmoja wa jamaa yake wala wa rafiki zake;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tu alipoanza kutawala na kuketi juu ya kiti cha ufalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tu alipoanza kutawala na kuketi juu ya kiti cha ufalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, alipoanza kutawala, mara alipoketi juu ya kiti chake cha enzi, akawaua nyumba yote ya Baasha; hakumwachia mwanamume yeyote, wa jamaa zake, wala wa rafiki zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tu alipoanza kutawala, Zimri aliwaua watu wote wa jamaa ya Baasha; hakumwachia hata mwanamume mmoja wa jamaa yake wala wa rafiki zake;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kuwa mfalme na kukaa katika kiti chake cha kifalme, akawaua wote waliokuwa wa mlango wa Basa, hakusaza wa kiume hata mmoja, wala ndugu zake, wala rafiki zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, alipoanza kutawala, mara alipoketi juu ya kiti chake cha enzi, akawaua nyumba yote ya Baasha; hakumwachia mwanamume ye yote, wa jamaa zake, wala wa rafiki zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara tu alipoanza kutawala, Simuri aliwaua watu wote wa jamaa ya Basha. Hakumwacha hata mwanaume mumoja wa jamaa yake wala warafiki zake.