1 Kings 16:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zimri alitawala huko Israeli kutoka Tirza kwa muda wa siku saba. Huo ulikuwa mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda. Basi, watu wa Israeli walikuwa wamepiga kambi kuuzingira mji wa Gibethoni wa Wafilisti,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala huko Tirsa siku saba. Jeshi lilikuwa limepiga kambi karibu na Gibethoni, mji wa Wafilisti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala muda wa siku saba huko Tirza. Basi, watu walikuwa wametua maragoni kupigana na Gibethoni, ulio wa Wafilisti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zimri alitawala huko Israeli kutoka Tirza kwa muda wa siku saba. Huo ulikuwa mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda. Basi, watu wa Israeli walikuwa wamepiga kambi kuuzingira mji wa Gibethoni wa Wafilisti,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa ishirini na saba wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala huko Tirza siku saba. Jeshi lilikuwa limepiga kambi karibu na Gibethoni, mji wa Wafilisti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala huko Tirsa siku saba. Jeshi lilikuwa limepiga kambi karibu na Gibethoni, mji wa Wafilisti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala muda wa siku saba huko Tirza. Basi, watu walikuwa wametua kambini kupigana na Gibethoni, ulio wa Wafilisti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zimri alitawala huko Israeli kutoka Tirza kwa muda wa siku saba. Huo ulikuwa mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda. Basi, watu wa Israeli walikuwa wamepiga kambi kuuzingira mji wa Gibethoni wa Wafilisti,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa 27 wa Asa, mfalme wa Wayuda, Zimuri akapata kuwa mfalme huko Tirsa siku 7; nao watu walikuwa wakiuzinga Gibetoni ulioko kwa Wafilisti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala muda wa siku saba huko Tirza. Basi, watu walikuwa wametua maragoni kupigana na Gibethoni, ulio wa Wafilisti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simuri alitawala kule Israeli akiwa Tirza kwa muda wa siku saba. Huo ulikuwa mwaka wa makumi mbili na saba wa utawala wa Asa mufalme wa Yuda. Watu wa Israeli walikuwa wamepiga kambi kwa kushambulia muji wa Gibetoni wa Wafilistini.