1 Kings 16:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Israeli, sasa, waligawanyika makundi mawili: Kundi moja lilimtambua Tibni mwana wa Ginathi kuwa mfalme, na kundi la pili lilimtambua Omri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha, watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamuunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme, na nusu nyingine wakamuunga mkono Omri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo watu wa Israeli wakatengwa sehemu mbili; nusu ya watu wakamfuata Tibni mwana wa Ginathi, ili wamfanye mfalme; nusu wakamfuata Omri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Israeli, sasa, waligawanyika makundi mawili: kundi moja lilimtambua Tibni mwana wa Ginathi kuwa mfalme, na kundi la pili lilimtambua Omri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamwunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme na nusu nyingine wakamwunga mkono Omri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamuunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme na nusu nyingine wakamuunga mkono Omri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo watu wa Israeli wakagawanywa sehemu mbili; nusu ya watu wakamfuata Tibni mwana wa Ginathi, ili wamfanye mfalme; nusu wakamfuata Omri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Israeli, sasa, waligawanyika makundi mawili: Kundi moja lilimtambua Tibni mwana wa Ginathi kuwa mfalme, na kundi la pili lilimtambua Omri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile wao walio ukoo wa Waisiraeli wakagawanyika kuwa pande mbili: nusu ya watu ikawa upande wa Tibuni, mwana wa Ginati, wamfanye kuwa mfalme, nusu yao ikawa upande wa Omuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo watu wa Israeli wakatengwa sehemu mbili; nusu ya watu wakamfuata Tibni mwana wa Ginathi, ili wamfanye mfalme; nusu wakamfuata Omri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, watu wa Israeli waligawanyika kwa makundi mawili: kundi moja lilimutambua Tibuni mwana wa Ginati kuwa mufalme, na kundi la pili lilimutambua Omuri.