1 Kings 16:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alinunua mlima wa Samaria kwa vipande 6,000 vya fedha kutoka kwa mtu mmoja aitwaye Shemeri, akajenga ngome juu yake, na mji. Mji wenyewe akauita Samaria, kwa heshima ya Shemeri aliyeumiliki mlima huo hapo awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akanunua kilima cha Samaria kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha; akajenga juu ya kilima kile, akauita mji alioujenga Samaria, kwa kuliandama jina lake Shemeri, aliyekuwa mwenye kilima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alinunua mlima wa Samaria kwa vipande 6,000 vya fedha kutoka kwa mtu mmoja aitwaye Shemeri, akajenga ngome juu yake, na mji. Mji wenyewe akauita Samaria, kwa heshima ya Shemeri aliyeumiliki mlima huo hapo awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akanunua kilima cha Samaria kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha; akajenga juu ya kilima kile, akauita mji alioujenga Samaria, kwa kufuata jina lake Shemeri, aliyekuwa mwenye kilima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alinunua mlima wa Samaria kwa vipande 6,000 vya fedha kutoka kwa mtu mmoja aitwaye Shemeri, akajenga ngome juu yake, na mji. Mji wenyewe akauita Samaria, kwa heshima ya Shemeri aliyeumiliki mlima huo hapo awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akaununua mlima wa Samaria kwa Semeri na kumlipa vipande viwili vya fedha, ndio shilingi 24000, kisha akajenga mji huko mlimani; nao huo mji, alioujenga, akauita Samaria kwa jina la Semeri aliyekuwa mwenye huo mlima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akanunua kilima cha Samaria kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha; akajenga juu ya kilima kile, akauita mji alioujenga Samaria, kwa kuliandama jina lake Shemeri, aliyekuwa mwenye kilima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alinunua mulima wa Samaria kwa vikoroti elfu sita vya feza kutoka kwa mutu mumoja anayeitwa Semeri, akajenga muji wenye kuta juu yake. Muji wenyewe akauita Samaria, kwa heshima ya Semeri aliyekuwa mwenyeji wa mulima huo hapo zamani.