1 Kings 16:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa utawala wake, Hieli kutoka Betheli, aliujenga upya mji wa Yeriko. Na sawa kabisa na neno la Mwenyezi-Mungu alilonena kwa njia ya Yoshua mwana wa Nuni, Hieli alifiwa na mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, wakati wa kuiweka misingi ya Yeriko, akafiwa pia na mwanawe mdogo Segubu, wakati wa kuyaweka malango yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa Ahabu, Hieli ule Mbetheli, akaijenga Yeriko upya. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kama Mwenyezi Mungu alivyonena kupitia kwa Yoshua, mwana wa Nuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa utawala wake, Hieli kutoka Betheli, aliujenga upya mji wa Yeriko. Na sawa kabisa na neno la Mwenyezi-Mungu alilonena kwa njia ya Yoshua mwana wa Nuni, Hieli alifiwa na mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, wakati wa kuiweka misingi ya Yeriko, akafiwa pia na mwanawe mdogo Segubu, wakati wa kuyaweka malango yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika wakati wa Ahabu, Hieli, Mbetheli, akaijenga upya Yeriko. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kulingana na neno la BWANA alilosema kupitia Yoshua mwana wa Nuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika wakati wa Ahabu, Hieli, Mbetheli, akaijenga upya Yeriko. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kulingana na neno la bwana alilosema kupitia Yoshua mwana wa Nuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wa utawala wake, Hieli kutoka Betheli, aliujenga upya mji wa Yeriko. Na sawa kabisa na neno la Mwenyezi-Mungu alilonena kwa njia ya Yoshua mwana wa Nuni, Hieli alifiwa na mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, wakati wa kuiweka misingi ya Yeriko, akafiwa pia na mwanawe mdogo Segubu, wakati wa kuyaweka malango yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizo siku zake Hieli wa Beteli akaujenga tena mji wa Yeriko. Alipoiweka misingi yake, Abiramu, mwanawe wa kwanza, akafa, tena alipoyatia malango, akafa mwanawe mdogo Segubu, kama Bwana alivyosema kinywani mwa Yosua, mwana wa Nuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa utawala wake, Hieli wa muji wa Beteli aliujenga upya muji wa Yeriko. Na sawa kabisa na neno Yawe alilosema kwa njia ya Yoshua mwana wa Nuni, Hieli alikufiwa na muzaliwa wake wa kwanza aliyeitwa Abiramu, wakati wa kuiweka misingi ya Yeriko. Akakufiwa vilevile na mwana wake mudogo aliyeitwa Segubu, wakati wa kuweka milango ya muji wa Yeriko.