1 Kings 16:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena neno la Mwenyezi-Mungu dhidi ya Baasha na jamaa yake, lilimjia Yehu mwanawe Hanani kwa sababu ya maovu aliyotenda mbele ya Mwenyezi-Mungu. Baasha alimkasirisha Mwenyezi-Mungu kwa matendo yake; alimwiga Yeroboamu na jamaa yake na kuiletea jamaa yake maangamizi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa nabii Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni pa Mwenyezi Mungu, akimkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu aliyoiangamiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena neno la Bwana likaja kwa mkono wa nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, na juu ya nyumba yake, kwa sababu ya mabaya yote aliyoyatenda machoni pa Bwana, akimghadhibisha kwa kazi ya mikono yake, kwa kufanana na nyumba ya Yeroboamu, na kwa sababu aliiharibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena neno la Mwenyezi-Mungu dhidi ya Baasha na jamaa yake, lilimjia Yehu mwanawe Hanani kwa sababu ya maovu aliyotenda mbele ya Mwenyezi-Mungu. Baasha alimkasirisha Mwenyezi-Mungu kwa matendo yake; alimwiga Yeroboamu na jamaa yake na kuiletea jamaa yake maangamizi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, neno la BWANA likamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni pa BWANA, akamkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu, na pia kwa sababu aliiangamiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, neno la bwana likamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa nabii Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni pa bwana, akamkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu, na pia kwa sababu aliiangamiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena neno la BWANA likaja kwa mkono wa nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, na juu ya nyumba yake, kwa sababu ya mabaya yote aliyoyatenda machoni pa BWANA, akimghadhibisha kwa kazi ya mikono yake, kwa kufanana na nyumba ya Yeroboamu, na kwa sababu aliiharibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena neno la Mwenyezi-Mungu dhidi ya Baasha na jamaa yake, lilimjia Yehu mwanawe Hanani kwa sababu ya maovu aliyotenda mbele ya Mwenyezi-Mungu. Baasha alimkasirisha Mwenyezi-Mungu kwa matendo yake; alimwiga Yeroboamu na jamaa yake na kuiletea jamaa yake maangamizi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno lile, Bwana alilolitoa kinywani mwa mfumbuaji Yehu, mwana wa Hanani, la mambo yatakayompata Basa na mlango wake, alilisema kwa ajili ya mabaya yote, aliyoyafanya machoni pa Bwana, amchafue kwa matendo ya mikono yake, akiwa kama wao wa mlango wa Yeroboamu, tena kwa kuwa aliwaua wao wa mlango wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena neno la BWANA likaja kwa mkono wa nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, na juu ya nyumba yake, kwa sababu ya mabaya yote aliyoyatenda machoni pa BWANA, akimghadhibisha kwa kazi ya mikono yake, kwa kufanana na nyumba ya Yeroboamu, na kwa sababu aliiharibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, neno la Yawe lilifika kwa njia ya nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Basha na jamaa yake, kwa sababu ya maovu aliyotenda mbele ya Yawe. Basha alimukasirikisha Yawe kwa matendo yake; alimwiga Yeroboamu na jamaa yake na kuiletea jamaa yake maangamizi.