1 Kings 16:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumishi wake Zimri ambaye alisimamia nusu ya kikosi cha magari yake ya kukokotwa, alikula njama juu yake. Siku moja, mfalme Ela alipokuwa huko Tirza nyumbani kwa Arsa aliyekuwa msimamizi wa ikulu, alikunywa, akalewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akapanga njama dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirsa, akilewa katika nyumba ya Arsa, aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirsa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamfanyia fitina; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumishi wake Zimri ambaye alisimamia nusu ya kikosi cha magari yake ya kukokotwa, alikula njama juu yake. Siku moja, mfalme Ela alipokuwa huko Tirza nyumbani kwa Arsa aliyekuwa msimamizi wa ikulu, alikunywa, akalewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akafanya hila mbaya dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akilewa katika nyumba ya Arsa, mtu aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akafanya hila mbaya dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirsa, akilewa katika nyumba ya Arsa, mtu aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirsa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamlia njama; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumishi wake Zimri ambaye alisimamia nusu ya kikosi cha magari yake ya kukokotwa, alikula njama juu yake. Siku moja, mfalme Ela alipokuwa huko Tirza nyumbani kwa Arsa aliyekuwa msimamizi wa ikulu, alikunywa, akalewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtumishi wake Zimuri, mkuu wa nusu ya magari, alipomlia njama; naye alikaa Tirsa. Siku moja alipokunywa na kulewa nyumbani mwa Arsa aliyekuwa mkuu wa nyumbani huko Tirsa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamfanyia fitina; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jemadari wake Simuri ambaye alisimamia nusu ya kundi ya magari yake ya vita alimwasi. Siku moja, mufalme Ela alipokuwa kule Tirza katika nyumba ya Arsa aliyekuwa musimamizi wa nyumba ya kifalme, alikunywa, akalewa.