1 Kings 17:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Elia akaondoka, akaenda Sarefathi. Alipofika penye lango la mji, alimkuta mwanamke mmoja mjane anaokota kuni. Elia akamwita mwanamke huyo na kumwambia “Niletee maji ninywe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, alimkuta mjane akiokota kuni pale. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Elia akaondoka, akaenda Sarefathi. Alipofika penye lango la mji, alimkuta mwanamke mmoja mjane anaokota kuni. Elia akamwita mwanamke huyo na kumwambia “Niletee maji ninywe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Elia akaondoka, akaenda Sarefathi. Alipofika penye lango la mji, alimkuta mwanamke mmoja mjane anaokota kuni. Elia akamwita mwanamke huyo na kumwambia “Niletee maji ninywe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akainuka, akaenda Sareputa. Alipofika penya lango la mji akaona huko mwanamke mjane aliyeokota kuni, akamwita na kumwambia: Uniletee maji kidogo katika kata, ninywe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Elia akaondoka, akaenda Zerepata. Alipofika kwenye mulango wa muji, akamukuta mwanamuke mumoja mujane akiokota kuni. Elia akamwita mwanamuke huyo na kumwambia: “Uniletee maji nikunywe.”