1 Kings 17:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mwanamke akamwambia, “Nakuapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wako aliye hai, sina mkate hata kidogo. Nilicho nacho ni konzi ya unga katika chungu na mafuta kidogo katika chupa. Nimefika hapa kuokota kuni, kisha niende nyumbani kupika chakula hicho, mwanangu na mimi tule, kisha tufe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamjibu, “Hakika kama Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aishivyo, sina mkate wowote, isipokuwa konzi moja ya unga kwenye chungu, na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili tule, kiishe, tukafe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mwanamke akamwambia, “Nakuapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wako aliye hai, sina mkate hata kidogo. Nilicho nacho ni konzi ya unga katika chungu na mafuta kidogo katika chupa. Nimefika hapa kuokota kuni, kisha niende nyumbani kupika chakula hicho, mwanangu na mimi tule, kisha tufe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamjibu, “Hakika kama BWANA Mungu wako aishivyo, sina mkate wo wote, isipokuwa konzi ya unga kwenye gudulia na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili kwamba tule, kiishe, tukafe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamjibu, “Hakika kama bwana Mwenyezi Mungu wako aishivyo, sina mkate wowote, isipokuwa konzi ya unga kwenye gudulia na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili kwamba tule, kiishe, tukafe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie mwenyewe na mwanangu, tule kisha tufe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mwanamke akamwambia, “Nakuapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wako aliye hai, sina mkate hata kidogo. Nilicho nacho ni konzi ya unga katika chungu na mafuta kidogo katika chupa. Nimefika hapa kuokota kuni, kisha niende nyumbani kupika chakula hicho, mwanangu na mimi tule, kisha tufe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamjibu: Hivyo, Bwana Mungu wako alivyo Mwenye uzima, sinacho kilichochomwa! Nilivyo navyo ndio gao la unga katika kitungi na vifuta vichache katika kichupa. Tazama, ninaokota vikuni viwili, nije nijipikie mwenyewe na mwanangu, tule, kisha tufe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo mwanamuke akamwambia: “Kama vile Yawe Mungu wako anavyoishi, sina mukate hata kidogo. Niko tu na unga unaoweza kujaa mukono mumoja katika chungu na mafuta kidogo katika chupa. Nimefika hapa kuokota kuni, kisha niende kwangu kupika chakula hicho, mwana wangu na mimi tukule, kisha tungojee kufa.”