1 Kings 17:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akamsihi Mwenyezi-Mungu akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, je, hata mwanamke huyu mjane ambaye ninakaa kwake, naye ananitunza, unamletea balaa kwa kumwua mwanawe?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akamlilia Mwenyezi Mungu, akasema “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi kwake, kwa kusababisha mwanawe kufa?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumfisha mwanawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akamsihi Mwenyezi-Mungu akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, je, hata mwanamke huyu mjane ambaye ninakaa kwake, naye ananitunza, unamletea balaa kwa kumwua mwanawe?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akamlilia BWANA, akasema “Ee BWANA Mungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi pamoja naye, kwa kusababisha mwanawe kufa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akamlilia bwana, akasema “Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi pamoja naye, kwa kusababisha mwanawe kufa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwomba BWANA, akanena, Ee BWANA, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumwua mwanawe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akamsihi Mwenyezi-Mungu akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, je, hata mwanamke huyu mjane ambaye ninakaa kwake, naye ananitunza, unamletea balaa kwa kumwua mwanawe?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamlilia Bwana kwamba: Bwana Mungu wangu, mbona umemfanyizia vibaya naye huyu mwanamke, ambaye nimefikia kwake, ukimwua mwanawe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwomba BWANA, akanena, Ee BWANA, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumfisha mwanawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akamusihi Yawe akisema: “Ee Yawe, Mungu wangu, hata mwanamuke huyu mujane ambaye ninakaa kwake, naye ananitunza, unamuletea hasara kwa kumwua mwana wake?”