1 Kings 18:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninahofia kwamba mara nitakapoondoka, Roho ya Mwenyezi-Mungu itakunyakua na kukupeleka mahali nisipopajua! Nikienda kumwambia Ahabu kwamba uko hapa, naye akikutafuta asikupate, ataniua mimi, ingawaje mimi mtumishi wako nimemcha Mwenyezi-Mungu tangu ujana wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sijui ni wapi Roho wa Mwenyezi Mungu ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua; lakini mimi mtumishi wako nimekuwa nikimwabudu Mwenyezi Mungu tangu ujana wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, roho ya Bwana atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha Bwana tangu ujana wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninahofia kwamba mara nitakapoondoka, Roho ya Mwenyezi-Mungu itakunyakua na kukupeleka mahali nisipopajua! Nikienda kumwambia Ahabu kwamba uko hapa, naye akikutafuta asikupate, ataniua mimi, ingawaje mimi mtumishi wako nimemcha Mwenyezi-Mungu tangu ujana wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sijui ni wapi Roho wa BWANA ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Kama nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua. Hata hivyo mimi mtumishi wako nimemwabudu BWANA tangu ujana wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sijui ni wapi Roho wa bwana ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Kama nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua. Hata hivyo mimi mtumishi wako nimemwabudu bwana tangu ujana wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, Roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninahofia kwamba mara nitakapoondoka, Roho ya Mwenyezi-Mungu itakunyakua na kukupeleka mahali nisipopajua! Nikienda kumwambia Ahabu kwamba uko hapa, naye akikutafuta asikupate, ataniua mimi, ingawaje mimi mtumishi wako nimemcha Mwenyezi-Mungu tangu ujana wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nitakapokwenda kutoka kwako, kisha Roho ya Bwana itakupeleka mahali, nisipopajua, nami nikienda kumpasha Ahabu hiyo habari, basi, asipokuona hataniua? Nami mtumishi wako ninamwogopa Bwana tangu ujana wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaogopa kwamba mara tu nitakapoondoka, Roho wa Yawe atakunyanyua na kukupeleka pahali nisipopajua! Nikienda kumwambia Ahabu kwamba uko hapa, naye akikutafuta na asikupate, ataniua mimi, ingawa mimi mutumishi wako ninamwogopa Yawe tangu ujana wangu.