1 Kings 18:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, huna habari kwamba Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, mimi niliwaficha manabii 100, watu hamsinihamsini pangoni, nikawa nawapa chakula na maji?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa Mwenyezi Mungu? Niliwaficha manabii wa Mwenyezi Mungu mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, na nikawapatia chakula na maji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Bwana wangu hakuambiwa nilivyofanya hapo Yezebeli alipowaua manabii wa Bwana? Jinsi nilivyowaficha manabii wa Bwana, watu mia, hamsini hamsini katika pango, nikawalisha chakula na kuwapa maji?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, huna habari kwamba Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, mimi niliwaficha manabii 100, watu hamsinihamsini pangoni, nikawa nawapa chakula na maji?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini wakati Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa BWANA? Niliwaficha manabii wa BWANA mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, nami nikawapatia chakula na maji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini wakati Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa bwana? Niliwaficha manabii wa bwana mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, nami nikawapatia chakula na maji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Bwana wangu hakuambiwa nilivyofanya hapo Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA? Jinsi nilivyowaficha manabii wa BWANA, watu mia moja, hamsini hamsini katika pango, nikawalisha chakula na kuwapa maji?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, huna habari kwamba Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, mimi niliwaficha manabii 100, watu hamsinihamsini pangoni, nikawa nawapa chakula na maji?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe bwana wangu, hukuambiwa niliyoyafanya, Izebeli alipowaua wafumbuaji wa Bwana, ya kuwa mia yao hao wafumbuaji wa Bwana nimewaficha hamsini hamsini pangoni, nikawapa mikate na maji?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Bwana wangu hakuambiwa nilivyofanya hapo Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA? Jinsi nilivyowaficha manabii wa BWANA, watu mia, hamsini hamsini katika pango, nikawalisha chakula na kuwapa maji?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hauna habari kwamba Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa Yawe, mimi niliwatwaa manabii mia moja nikawaficha makumi tano tano katika pango, nikakuwa ninawapatia chakula na maji?