1 Kings 18:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Elia akawakaribia watu hao, akawaambia, “Mtasitasita na kuyumbayumba mioyoni mpaka lini? Ikiwa Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu mfuateni; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi, mfuateni yeye.” Lakini watu hawakumjibu neno lolote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtayumbayumba katikati ya mawazo mawili hadi lini? Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.” Lakini watu hawakusema kitu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Elia akawakaribia watu hao, akawaambia, “Mtasitasita na kuyumbayumba mioyoni mpaka lini? Ikiwa Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu mfuateni; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi, mfuateni yeye.” Lakini watu hawakumjibu neno lolote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eliya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtasitasita katika mawazo mawili hadi lini? Ikiwa BWANA ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.” Lakini watu hawakusema kitu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtasitasita katika mawazo mawili hadi lini? Ikiwa bwana ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.” Lakini watu hawakusema kitu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Elia akawakaribia watu hao, akawaambia, “Mtasitasita na kuyumbayumba mioyoni mpaka lini? Ikiwa Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu mfuateni; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi, mfuateni yeye.” Lakini watu hawakumjibu neno lolote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elia akafika huko, watu wote waliko, akawaambia: Mpaka lini mtakwenda na kuchechemea pande mbili? Kama Bwana ni Mungu, mfuateni! Kama Baali ni Mungu, mfuateni! Lakini watu hawakumjibu neno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Elia akawakaribia watu hao, akawaambia: “Mutaendelea kusitasita ndani ya mioyo mpaka wakati gani? Ikiwa Yawe ni Mungu, mumufuate; lakini ikiwa Bali ni Mungu, basi, mumufuate.” Lakini watu hawakumujibu neno lolote.