1 Kings 18:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya! Leteni fahali wawili; manabii wa Baali wajichagulie fahali mmoja, wamchinje, wamkate vipandevipande na kumweka juu ya kuni, bila kuwasha moto. Nami pia nitamtwaa huyo fahali mwingine, nitamchinja na kumweka juu ya kuni bila kuwasha moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na wamweke juu ya kuni, lakini wasimwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni, lakini sitamwashia moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie ng'ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya! Leteni fahali wawili; manabii wa Baali wajichagulie fahali mmoja, wamchinje, wamkate vipandevipande na kumweka juu ya kuni, bila kuwasha moto. Nami pia nitamtwaa huyo fahali mwingine, nitamchinja na kumweka juu ya kuni bila kuwasha moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na waweke juu ya kuni lakini wasiiwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni lakini sitawasha moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na waweke juu ya kuni lakini wasiiwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni lakini sitawasha moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie ng'ombe mmoja, wamkatekate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya! Leteni fahali wawili; manabii wa Baali wajichagulie fahali mmoja, wamchinje, wamkate vipandevipande na kumweka juu ya kuni, bila kuwasha moto. Nami pia nitamtwaa huyo fahali mwingine, nitamchinja na kumweka juu ya kuni bila kuwasha moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na tupewe ng'ombe wawili, nao wajichagulie dume mmoja, wamkatekate, wamweke juu ya chungu ya kuni, lakini wasitie moto! Nami nitamfanyizia yule dume mwingine vivyo hivyo, kisha nimweke juu ya chungu ya kuni, lakini moto sitatia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo na watutolee ng’ombe wawili; wao na wajichagulie ng’ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza huyo ng’ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi! Mulete ngombe dume wawili. Manabii wa Bali wajichagulie ngombe dume mumoja, wamuchinje, wamukate vipandevipande na kumuweka juu ya kuni, bila kuwasha moto. Nami vilevile nitamutwaa yule ngombe dume mwingine, nitamuchinja na kumuweka juu ya kuni bila kuwasha moto.