1 Kings 18:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Elia akawaambia manabii wa Baali, “Nyinyi ni wengi; basi anzeni. Jichagulieni fahali, mtayarisheni na kumwomba mungu wenu, lakini msiwashe moto.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na mwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Elia akawaambia manabii wa Baali, “Nyinyi ni wengi; basi anzeni. Jichagulieni fahali, mtayarisheni na kumwomba mungu wenu, lakini msiwashe moto.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eliya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na muwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na mwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Elia akawaambia manabii wa Baali, “Nyinyi ni wengi; basi anzeni. Jichagulieni fahali, mtayarisheni na kumwomba mungu wenu, lakini msiwashe moto.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Elia akawaambia watambikaji wa Baali: Jichagulieni dume mmoja, mwanze kumtengeneza! Kwani ninyi m wengi. Kisha litambikieni jina la mungu wenu, lakini moto msitie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng’ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Elia akawaambia manabii wa Bali: “Ninyi ni wengi. Basi, muanze. Mujichagulie, mutayarishe ngombe dume, mumutayarishe na kumwomba mungu wenu, lakini musiwashe moto.”