1 Kings 18:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Manabii hao wakapiga kelele zaidi, wakajikatakata kwa visu na simi, kufuatana na desturi yao, hata wakabubujika damu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja kwa visu na vyembe, hadi damu ikachuruzika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Manabii hao wakapiga kelele zaidi, wakajikatakata kwa visu na simi, kufuatana na desturi yao, hata wakabubujika damu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja wenyewe kwa visu na vyembe, mpaka damu ikachuruzika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja wenyewe kwa visu na vyembe, mpaka damu ikachuruzika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakapiga kelele, wakajikatakata kwa visu na nyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Manabii hao wakapiga kelele zaidi, wakajikatakata kwa visu na simi, kufuatana na desturi yao, hata wakabubujika damu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakapaza sauti sana za kumwita, wakajichanjachanja kwa mapanga na kwa visu kama desturi yao, hata damu zikawatoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manabii hao wakapiga kelele zaidi, wakajikatakata kwa visu na wembe, kufuatana na desturi yao, hata damu ikawatiririka.