1 Kings 18:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa mawe hayo, Elia alimjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu, akachimba na mtaro kuizunguka madhabahu hiyo; mtaro uwezao kuchukua kama debe moja na nusu la nafaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina la Mwenyezi Mungu, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa mawe hayo, Elia alimjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu, akachimba na mtaro kuizunguka madhabahu hiyo; mtaro uwezao kuchukua kama debe moja na nusu la nafaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina la BWANA, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina la bwana, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa mawe hayo, Elia alimjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu, akachimba na mtaro kuizunguka madhabahu hiyo; mtaro uwezao kuchukua kama debe moja na nusu la nafaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo mawe akayajenga na kulitaja Jina la Bwana, pawe pa kutambikia, kisha akachimba mfereji wenye upana wa shamba litoshalo kumyagia humo pishi mbili za mbegu, ukapazunguka hapo pa kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mawe hayo, Elia alimujengea Yawe mazabahu. Akachimba mufereji pembenipembeni ya mazabahu hiyo, mufereji ambao unaweza kujazwa na maji yapata litre kumi na ine.