1 Kings 18:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo alasiri, wakati wa kutoa tambiko, nabii Elia aliikaribia madhabahu, akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, waoneshe watu leo hii kwamba wewe ndiwe Mungu wa Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya kwa amri yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Ilya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kama ulivyoagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo alasiri, wakati wa kutoa tambiko, nabii Elia aliikaribia madhabahu, akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, waoneshe watu leo hii kwamba wewe ndiwe Mungu wa Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya kwa amri yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Ilya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee bwana, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo alasiri, wakati wa kutoa tambiko, nabii Elia aliikaribia madhabahu, akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, waoneshe watu leo hii kwamba wewe ndiwe Mungu wa Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya kwa amri yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipotolea vilaji vya tambiko, mfumbuaji Elia akatokea, akasema: Bwana, Mungu wa Aburahamu na wa Isaka na wa Isiraeli, leo hivi na yajulikane, ya kuwa wewe ndiwe Mungu kwao Waisiraeli, mimi nami ndimi mtumishi wako. Tena kwa neno lako nimeyafanya haya yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa wakati wa kutoa sadaka ya magaribi, nabii Elia aliikaribia mazabahu, akaomba: “Ee Yawe, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, uwaonyeshe watu leo hii kwamba wewe ndiwe Mungu wa Israeli, na kwamba mimi ni mutumishi wako na nimefanya mambo haya kwa amri yako.