1 Kings 18:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na wakati Yezebeli alipowaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, Obadia aliwachukua manabii 100, akawaficha hamsinihamsini pangoni, akawa anawapelekea chakula na maji).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa Mwenyezi Mungu, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja, na akawa akiwapa chakula na maji.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa Bwana, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na wakati Yezebeli alipowaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, Obadia aliwachukua manabii 100, akawaficha hamsinihamsini pangoni, akawa anawapelekea chakula na maji).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa BWANA, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja na akawa anawapatia chakula na maji.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa bwana, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja na akawa akiwapa chakula na maji.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia moja, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na wakati Yezebeli alipowaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, Obadia aliwachukua manabii 100, akawaficha hamsinihamsini pangoni, akawa anawapelekea chakula na maji).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, Izebeli alipowaangamiza wafumbuaji wa Bwana, Obadia alichukua wafumbuaji mia, akawaficha hamsini hamsini pangoni, akawatunza na kuwapa mikate na maji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na wakati Yezebeli alipowaua manabii wa Yawe, Obadia aliwachukua manabii mia moja, akawaficha makumi tano tano ndani ya pango, akakuwa anawapelekea chakula na maji.