1 Kings 18:44 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara ya saba, huyo mtumishi akarudi, akasema, “Naona wingu dogo kama mkono wa mtu linatoka baharini.” Elia akamwambia, “Nenda umwambie mfalme Ahabu atayarishe gari lake la kukokotwa, ateremke, asije akazuiliwa na mvua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, “Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini.” Hivyo Ilya akasema, “Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako la vita, ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara ya saba, huyo mtumishi akarudi, akasema, “Naona wingu dogo kama mkono wa mtu linatoka baharini.” Elia akamwambia, “Nenda umwambie mfalme Ahabu atayarishe gari lake la kukokotwa, ateremke, asije akazuiliwa na mvua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, “Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini.” Hivyo Eliya akasema, “Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, “Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini.” Hivyo Ilya akasema, “Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Nenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara ya saba, huyo mtumishi akarudi, akasema, “Naona wingu dogo kama mkono wa mtu linatoka baharini.” Elia akamwambia, “Nenda umwambie mfalme Ahabu atayarishe gari lake la kukokotwa, ateremke, asije akazuiliwa na mvua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika mara ya saba akasema: Nimeona kiwingu kidogo kama kiganja cha mtu, kinatoka baharini. Akamwambia: Nenda kumwambia Ahabu: Tandika farasi, ushuke upesi, mvua isikuzuie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mara ya saba, yule mutumishi akarudia, akasema: “Ninaona wingu dogo kama mukono wa mutu linatoka katika bahari.” Elia akamwambia: “Kwenda umwambie mufalme Ahabu atayarishe gari lake la vita, ateremuke, asipate kuzuiliwa na mvua.”