1 Kings 18:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Ahabu akamwambia Obadia, “Labda tutapata majani na hapo tutawaokoa baadhi ya farasi na nyumbu wetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahabu alikuwa amemwambia Obadia, “Nenda katika nchi yote kwenye vijito vyote na mabonde. Huenda tunaweza kupata majani ya kuwalisha farasi na nyumbu ili wapate kuishi, tusilazimike kumuua hata mmoja wa wanyama wetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Ahabu akamwambia Obadia, “Labda tutapata majani na hapo tutawaokoa baadhi ya farasi na nyumbu wetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ahabu alikuwa amemwambia Obadia, “Nenda katika nchi yote kwenye vijito vyote na mabonde. Huenda tunaweza kupata majani ya kuwalisha farasi na nyumbu wapate kuishi ili tusilazimike kuwaua hata mmoja wa wanyama wetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ahabu alikuwa amemwambia Obadia, “Nenda katika nchi yote kwenye vijito vyote na mabonde. Huenda tunaweza kupata majani ya kuwalisha farasi na nyumbu wapate kuishi ili tusilazimike kuwaua hata mmoja wa wanyama wetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Ahabu akamwambia Obadia, “Labda tutapata majani na hapo tutawaokoa baadhi ya farasi na nyumbu wetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahabu akamwambia Obadia: Tembea katika nchi kwenye chemchemi zote za maji na kwenye vijito kutazama-tazama, kama majani yanapatikana ya kuwaponya farasi na punda njaa, tusifiwe na hawa nyama wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ahabu akamwambia Obadia: “Labda tutapata majani na pale tutaokoa farasi na nyumbu wetu wamoja.”