1 Kings 18:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Obadia alipokuwa njiani, alikutana na Elia; naye Obadia alipomtambua Elia, aliinama chini na kusema, “Kumbe! Ni wewe bwana wangu Elia?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Obadia alipokuwa akitembea njiani, Ilya akakutana naye. Obadia akamtambua, akasujudu, uso wake ukigusa chini, na kusema, “Je, hivi kweli ni wewe, bwana wangu Ilya?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Obadia alipokuwa njiani, kumbe! Eliya akakutana naye. Akamtambua, akaanguka kifudifudi, akanena, Je! Ni wewe, bwana wangu Eliya?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Obadia alipokuwa njiani, alikutana na Elia; naye Obadia alipomtambua Elia, aliinama chini na kusema, “Kumbe! Ni wewe bwana wangu Elia?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Obadia alipokuwa akitembea njiani, Eliya akakutana naye. Obadia akamtambua, akamsujudia hadi nchi na kusema, “Je, hivi kweli ni wewe, bwana wangu Eliya?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Obadia alipokuwa akitembea njiani, Ilya akakutana naye. Obadia akamtambua, akamsujudia hadi nchi na kusema, “Je, hivi kweli ni wewe, bwana wangu Ilya?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Obadia alipokuwa njiani, kumbe! Eliya akakutana naye. Akamtambua, akaanguka kifudifudi, akanena, Je! Ni wewe, bwana wangu Eliya?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Obadia alipokuwa njiani, alikutana na Elia; naye Obadia alipomtambua Elia, aliinama chini na kusema, “Kumbe! Ni wewe bwana wangu Elia?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Obadia alipofika njiani, mara akakutana na Elia; alipomtambua akamwangukia usoni pake, akamwambia: Kumbe wewe ndiwe bwana wangu Elia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Obadia alipokuwa njiani, kumbe! Eliya akakutana naye. Akamtambua, akaanguka kifudifudi, akanena, Je! Ni wewe, bwana wangu Eliya?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Obadia alipokuwa katika njia, alikutana na Elia; naye Obadia alipomutambua Elia, aliinama chini na kusema: “Hakika, ni wewe bwana wangu Elia?”