1 Kings 19:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tetemeko likapita, kukawa na moto. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika moto huo. Baada ya moto, pakatokea sauti ndogo, tulivu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya tetemeko la ardhi moto ukaja, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong’ona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tetemeko likapita, kukawa na moto. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika moto huo. Baada ya moto, pakatokea sauti ndogo, tulivu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakini BWANA hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong'ona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakini bwana hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong’ona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tetemeko likapita, kukawa na moto. Lakini Mwenyezi-Mungu hakuwemo katika moto huo. Baada ya moto, pakatokea sauti ndogo, tulivu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtetemeko ulipokwisha pita, pakafuata moto, lakini namo motoni Bwana hakuwamo. Moto ulipokwisha pita, pakaja sauti nyembamba yenye upole.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tetemeko likapita, kukakuwa moto. Lakini Yawe hakukuwa katika moto ule. Nyuma ya moto, kukatokea sauti ndogo, tulivu.