1 Kings 19:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Elisha akawaacha ng'ombe wake, akamfuata Elia mbio na kumwambia, “Niruhusu kwanza niende kumpa baba yangu na mama yangu busu la kwaheri, kisha nikufuate.” Elia akamjibu, “Nenda! Kwani nimekuzuia?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Al-Yasa akawaacha maksai wake, akamkimbilia Ilya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.” Ilya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekufanya nini?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akawaacha ng'ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Enenda, urudi; ni nini niliyokutendea?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Elisha akawaacha ng'ombe wake, akamfuata Elia mbio na kumwambia, “Niruhusu kwanza niende kumpa baba yangu na mama yangu busu la kwaheri, kisha nikufuate.” Elia akamjibu, “Nenda! Kwani nimekuzuia?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Elisha akawaacha maksai wake, akamkimbilia Eliya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.” Eliya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekutendea nini?.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Al-Yasa akawaacha maksai wake, akamkimbilia Ilya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.” Ilya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekutendea nini?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akawaacha ng'ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Nenda, urudi; ni nini niliyokutendea?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Elisha akawaacha ng'ombe wake, akamfuata Elia mbio na kumwambia, “Niruhusu kwanza niende kumpa baba yangu na mama yangu busu la kwaheri, kisha nikufuate.” Elia akamjibu, “Nenda! Kwani nimekuzuia?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowaacha ng'ombe wake, akamkimbilia Elia, akamwambia: Nipe ruhusa, kwanza ninoneane na baba na mama! Kisha nitakufuata. Akajibu: Nenda, uridi upesi! Usisahau niliyokutendea!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akawaacha ng’ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Enenda, urudi; ni nini niliyokutendea?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, Elisha akawaacha ngombe wake, akamufuata Elia mbio na kumwambia: “Uniruhusu kwanza niende kumupa baba yangu na mama yangu busu la kwa heri, kisha nikufuate.” Elia akamujibu: “Kwenda! Ni nini niliyokutendea?”