1 Kings 19:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
naye akatembea mwendo wa siku nzima kuingia jangwani. Basi, akafika, akaketi chini ya mti mmoja, mretemu. Hapo, akaomba afe, akisema, “Imetosha! Siwezi tena. Ee Mwenyezi-Mungu, sasa utoe uhai wangu. Mimi si bora kuliko wazee wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa, Mwenyezi Mungu, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
naye akatembea mwendo wa siku nzima kuingia jangwani. Basi, akafika, akaketi chini ya mti mmoja, mretemu. Hapo, akaomba afe, akisema, “Imetosha! Siwezi tena. Ee Mwenyezi-Mungu, sasa utoe uhai wangu. Mimi si bora kuliko wazee wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa, BWANA, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa, bwana, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
naye akatembea mwendo wa siku nzima kuingia jangwani. Basi, akafika, akaketi chini ya mti mmoja, mretemu. Hapo, akaomba afe, akisema, “Imetosha! Siwezi tena. Ee Mwenyezi-Mungu, sasa utoe uhai wangu. Mimi si bora kuliko wazee wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenyewe akaenda nyikani mwendo wa siku moja, akaja kukaa chini ya mfagio mmoja, akajiombea kufa akisema: Nimechoka sasa; Bwana, ichukue roho yangu! Kwani mimi si mwema kuliko baba zangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
naye akatembea mwendo wa siku nzima kuingia katika jangwa. Basi, akafika, akaikaa chini ya muti mumoja wa muretemu. Halafu, akaomba apate kufa, akisema: “Inatosha! Siwezi tena. Ee Yawe, sasa utoe uzima wangu. Mimi si bora kuliko babu zangu.”