1 Kings 2:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alikuwa ametawala Israeli kwa muda wa miaka arubaini; miaka saba akiwa Hebroni, na miaka thelathini na mitatu akiwa Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi alikuwa ametawala Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na tatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na siku alizotawala Daudi juu ya Israeli zilikuwa miaka arobaini; huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alikuwa ametawala Israeli kwa muda wa miaka arubaini; miaka saba akiwa Hebroni, na miaka thelathini na mitatu akiwa Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini, miaka saba huko Hebroni na miaka thelathini na mitatu katika Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na siku alizotawala Daudi juu ya Israeli zilikuwa miaka arobaini; huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alikuwa ametawala Israeli kwa muda wa miaka arubaini; miaka saba akiwa Hebroni, na miaka thelathini na mitatu akiwa Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo siku, Dawidi alizokuwa mfalme wa Waisiraeli, ni miaka 40; Heburoni alishika ufalme miaka 7, namo mle Yerusalemu alishika ufalme miaka 33.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na siku alizotawala Daudi juu ya Israeli zilikuwa miaka arobaini; huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alikuwa ametawala inchi ya Israeli kwa muda wa miaka makumi ine; miaka saba akiwa Hebroni, na miaka makumi tatu na mitatu akiwa Yerusalema.