1 Kings 2:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Adoniya akamwambia, “Unajua kwamba mimi ningalikuwa mfalme, na hata Israeli yote ilikuwa inanitazamia niwe mfalme. Lakini, mambo yakageuka na ndugu yangu akanipindua, kwani hayo ndio yaliyokuwa mapenzi yake Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, na ufalme umeenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili nimiliki mimi; walakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Adoniya akamwambia, “Unajua kwamba mimi ningalikuwa mfalme, na hata Israeli yote ilikuwa inanitazamia niwe mfalme. Lakini, mambo yakageuka na ndugu yangu akanipindua, kwani hayo ndio yaliyokuwa mapenzi yake Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili mimi nimiliki; lakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Adoniya akamwambia, “Unajua kwamba mimi ningalikuwa mfalme, na hata Israeli yote ilikuwa inanitazamia niwe mfalme. Lakini, mambo yakageuka na ndugu yangu akanipindua, kwani hayo ndio yaliyokuwa mapenzi yake Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Unajua, ya kuwa ufalme ulikuwa wangu, nao Waisiraeli wote walikuwa wakinielekezea nyuso zao, niwe mfalme; lakini tena ufalme ukageuka kuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake kwa agizo la Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili nimiliki mimi; walakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Adonia akamwambia: “Unajua kwamba ni mimi ndiye ningalikuwa mufalme, na hata Israeli yote ilikuwa inanitazamia nikuwe mufalme. Lakini, mambo yakageuka na ndugu yangu akanipindua, kwa sababu hayo ndiyo yaliyokuwa mapenzi ya Yawe.