1 Kings 2:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akasema, “Tafadhali, nakusihi umwombe mfalme Solomoni aniruhusu nimchukue Abishagi, yule Mshunami, awe mke wangu, kwa maana najua hatakukatalia wewe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Sulemani, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nena, nakusihi, na Sulemani, mfalme, (kwa kuwa hawezi kukukataza neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akasema, “Tafadhali, nakusihi umwombe mfalme Solomoni aniruhusu nimchukue Abishagi, yule Mshunami, awe mke wangu, kwa maana najua hatakukatalia wewe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Solomoni, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Sulemani, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nakusihi nena na Sulemani, mfalme (kwa kuwa hawezi kukukatalia neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akasema, “Tafadhali, nakusihi umwombe mfalme Solomoni aniruhusu nimchukue Abishagi, yule Mshunami, awe mke wangu, kwa maana najua hatakukatalia wewe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Sema na mfalme Salomo, kwani hatautweza uso wako, anipe Abisagi wa Sunemu, awe mke wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nena, nakusihi, na Sulemani, mfalme, (kwa kuwa hawezi kukukataza neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akasema: “Tafazali, ninakusihi umwombe mufalme Solomono aniruhusu nimukamate Abisagi, yule Musunami, akuwe muke wangu, kwa maana ninajua hatakukatalia wewe.”