1 Kings 2:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Solomoni akamwuliza mama yake, “Kwa nini unataka nimpe Abishagi? Hii ni sawa kabisa na kumtakia ufalme wangu! Kumbuka ya kwamba yeye ni kaka yangu mkubwa, na isitoshe, kuhani Abiathari na jemadari Yoabu mwana wa Seruya, wako upande wake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi Mshunami, kwa ajili ya Adoniya? Mwombee na ufalme pia kwani yeye ni ndugu yangu mkubwa: naam, kwa ajili yake, na kwa ajili ya kuhani Abiathari, na Yoabu mwana wa Seruya!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajibu mfalme Sulemani akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Solomoni akamwuliza mama yake, “Kwa nini unataka nimpe Abishagi? Hii ni sawa kabisa na kumtakia ufalme wangu! Kumbuka ya kwamba yeye ni kaka yangu mkubwa, na isitoshe, kuhani Abiathari na jemadari Yoabu mwana wa Seruya, wako upande wake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Solomoni akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi, Mshunami, kwa ajili ya Adonia? Ungeweza pia kuomba ufalme kwa ajili yake, hata hivyo, yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, pia kuhani Abiathari na Yoabu mwana wa Seruya wapo upande wake!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi, Mshunami, kwa ajili ya Adoniya? Ungeweza pia kuomba ufalme kwa ajili yake, kwani yeye ni ndugu yangu mkubwa: naam, kwa ajili yake, na kwa kuhani Abiathari na Yoabu mwana wa Seruya!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme Sulemani akajibu, akamwambia mamaye, Mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Solomoni akamwuliza mama yake, “Kwa nini unataka nimpe Abishagi? Hii ni sawa kabisa na kumtakia ufalme wangu! Kumbuka ya kwamba yeye ni kaka yangu mkubwa, na isitoshe, kuhani Abiathari na jemadari Yoabu mwana wa Seruya, wako upande wake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme Salomo akajibu akimwambia mama yake: Ni kwa sababu gani, ukimwombea Adonia, apewe Abisagi wa Sunemu? Umwombee nao ufalme! Kwani yeye ni ndugu yangu aliye mkubwa kuliko mimi. Waombee nao akina mtambikaji Abiatari na Yoabu, mwana wa Seruya!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajibu mfalme Sulemani akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Solomono akamwuliza mama yake: “Kwa nini unataka nimupe Abisagi? Hii ni sawa kabisa na kumutakia ufalme wangu! Kumbuka kwamba yeye ni mukubwa yangu, na si ile tu, kuhani Abiatari na jemadari Yoabu mwana wa Zeruya, wako upande wake!”