1 Kings 2:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Solomoni akamwambia kuhani Abiathari, “Ondoka uende shambani kwako, huko Anathothi; unastahili kufa wewe! Lakini sasa, sitakuua kwa sababu ulilishughulikia sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu ulipokuwa na baba yangu Daudi, ukateswa pamoja naye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku la Bwana Mungu Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, mfalme akamwambia Abiathari kuhani, Enenda Anathothi mashambani kwako; kwa kuwa wastahili kufa; ila leo sikuui, kwa sababu wewe ulichukua sanduku la Bwana mbele ya Daudi baba yangu, na kwa sababu wewe uliteswa kwa mateso yote ya baba yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Solomoni akamwambia kuhani Abiathari, “Ondoka uende shambani kwako, huko Anathothi; unastahili kufa wewe! Lakini sasa, sitakuua kwa sababu ulilishughulikia sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu ulipokuwa na baba yangu Daudi, ukateswa pamoja naye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku la BWANA Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku la bwana Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, mfalme akamwambia Abiathari kuhani, Nenda Anathothi mashambani kwako; kwa kuwa wastahili kufa; ila leo sikuui, kwa sababu wewe ulichukua sanduku la Bwana mbele ya Daudi baba yangu, na kwa sababu wewe uliteswa kwa mateso yote ya baba yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Solomoni akamwambia kuhani Abiathari, “Ondoka uende shambani kwako, huko Anathothi; unastahili kufa wewe! Lakini sasa, sitakuua kwa sababu ulilishughulikia sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu ulipokuwa na baba yangu Daudi, ukateswa pamoja naye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mtambikaji Abiatari mfalme akamwambia: Nenda Anatoti shambani kwako! Kwani wewe unapaswa na kufa; lakini leo hivi sitakuua, kwa kuwa ulilichukua Sanduku la Bwana Mungu mbele ya baba yangu Dawidi, tena ukateseka katika mateso yote yaliyompata baba yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, mfalme akamwambia Abiathari kuhani, Enenda Anathothi mashambani kwako; kwa kuwa wastahili kufa; ila leo sikuui, kwa sababu wewe ulichukua sanduku la Bwana mbele ya Daudi baba yangu, na kwa sababu wewe uliteswa kwa mateso yote ya baba yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Solomono akamwambia kuhani Abiatari: “Ondoka uende katika shamba lako, kule Anatoti. Unastahili kufa wewe. Lakini sasa, sitakuua kwa sababu ulilishugulikia Sanduku la Agano la Yawe ulipokuwa na baba yangu Daudi, ukateswa pamoja naye.”