1 Kings 2:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme Solomoni akamfukuza Abiathari, asiwe kuhani wa Mwenyezi-Mungu; hivyo likatimia neno alilosema Mwenyezi-Mungu huko Shilo, juu ya Eli na ukoo wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Sulemani akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa Mwenyezi Mungu, akilitimiza neno la Mwenyezi Mungu alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa Bwana; ili alitimize neno la Bwana, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme Solomoni akamfukuza Abiathari, asiwe kuhani wa Mwenyezi-Mungu; hivyo likatimia neno alilosema Mwenyezi-Mungu huko Shilo, juu ya Eli na ukoo wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Solomoni akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa BWANA, akilitimiza neno la BWANA alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Sulemani akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa bwana, akilitimiza neno la bwana alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa BWANA; ili alitimize neno la BWANA, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mfalme Solomoni akamfukuza Abiathari, asiwe kuhani wa Mwenyezi-Mungu; hivyo likatimia neno alilosema Mwenyezi-Mungu huko Shilo, juu ya Eli na ukoo wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Salomo alivyomfukuza Abiatari, asiwe tena mtambikaji wa Bwana; akalitimiza lile neno la Bwana, alilolisema la mlango wa Eli kule Silo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa BWANA; ili alitimize neno la BWANA, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mufalme Solomono akamufukuza Abiatari, asikuwe kuhani wa Yawe. Hivyo likatimia neno alilosema Yawe kule Shilo, juu ya Eli na ukoo wake.