1 Kings 2:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoabu alipopata habari, alikimbilia hemani mwa Mungu na kushikilia pembe za madhabahu; kwa maana alikuwa amemwunga mkono Adoniya na si Absalomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Habari zilipomfikia Yoabu, aliyekuwa amepanga njama na Adoniya, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema la Mwenyezi Mungu na kushika pembe za madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, habari zikamfikia Yoabu; kwa maana Yoabu alikuwa amemfuata Adonia, ingawa hakumfuata Absalomu. Yoabu akakimbilia Hemani kwa Bwana, akazishika pembe za madhabahu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoabu alipopata habari, alikimbilia hemani mwa Mungu na kushikilia pembe za madhabahu; kwa maana alikuwa amemwunga mkono Adoniya na si Absalomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Habari zilipomfikia Yoabu, ambaye alikuwa amefanya shauri baya na Adonia, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema la BWANA na kushika pembe za madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Habari zilipomfikia Yoabu, ambaye alikuwa amefanya shauri baya na Adoniya, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema la bwana na kushika pembe za madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, habari zikamfikia Yoabu; kwa maana Yoabu alikuwa amemfuata Adonia, ingawa hakumfuata Absalomu. Yoabu akakimbilia Hemani kwa BWANA, akazishika pembe za madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoabu alipopata habari, alikimbilia hemani mwa Mungu na kushikilia pembe za madhabahu; kwa maana alikuwa amemwunga mkono Adoniya na si Absalomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Habari hizi zikamfikia Yoabu, maana Yoabu alikuwa ameandamana na Adonia, ingawa Abisalomu hakuandamana naye kumfuata; ndipo, Yoabu alipokimbilia Hemani mwa Bwana, akazishika pembe za meza ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, habari zikamfikia Yoabu; kwa maana Yoabu alikuwa amemfuata Adonia, ingawa hakumfuata Absalomu. Yoabu akakimbilia Hemani kwa BWANA, akazishika pembe za madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoabu alipopata habari, alikimbilia katika hema ya Mungu na kushikilia pembe za mazabahu kwa maana alikuwa amemwunga Adonia mukono ingawa mbele hakukuwa na Abusaloma.