1 Kings 2:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Adhabu ya mauaji hayo itakuwa juu ya Yoabu na wazawa wake milele. Bali Mwenyezi-Mungu atawapa ufanisi daima, Daudi na wazawa wake watakaokalia kiti chake cha enzi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya Mwenyezi Mungu milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Adhabu ya mauaji hayo itakuwa juu ya Yoabu na wazawa wake milele. Bali Mwenyezi-Mungu atawapa ufanisi daima, Daudi na wazawa wake watakaokalia kiti chake cha enzi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya BWANA milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya bwana milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Adhabu ya mauaji hayo itakuwa juu ya Yoabu na wazawa wake milele. Bali Mwenyezi-Mungu atawapa ufanisi daima, Daudi na wazawa wake watakaokalia kiti chake cha enzi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Damu zao na zikirudie kichwa cha Yoabu na vichwa vya vizazi vyake kale na kale! Lakini kwake Dawidi na kwa vizazi vyake na kwa mlango wake na kwa kiti chake cha kifalme na kuweko kale na kale na matengemano yatokayo kwa Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Azabu ya mauaji hayo itakuwa juu ya Yoabu na wazao wake milele. Lakini Yawe atawabariki siku zote Daudi na wazao wake watakaoikalia kiti chake cha kifalme.”