1 Kings 2:42 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alimwita Shimei na kumwambia, “Je, hukuniapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu kwamba hutatoka Yerusalemu, nami sikukuonya kwa dhati kwamba, hakika utakufa kama utathubutu kwenda nje? Nawe ulikubali, ukaniambia, ‘Vema, nitatii.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa Mwenyezi Mungu na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa’? Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa Bwana, na kukushuhudia, kusema, Siku ile ya kutoka kwako ukienda mahali po pote, ujue hakika ya kwamba kufa utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alimwita Shimei na kumwambia, “Je, hukuniapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu kwamba hutatoka Yerusalemu, nami sikukuonya kwa dhati kwamba, hakika utakufa kama utathubutu kwenda nje? Nawe ulikubali, ukaniambia, ‘Vema, nitatii.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa BWANA na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine po pote, uwe na hakika utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa bwana na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa BWANA, na kukushuhudia, kusema, Siku ile utakapotoka ukaenda mahali popote, ujue kwamba hakika utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alimwita Shimei na kumwambia, “Je, hukuniapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu kwamba hutatoka Yerusalemu, nami sikukuonya kwa dhati kwamba, hakika utakufa kama utathubutu kwenda nje? Nawe ulikubali, ukaniambia, ‘Vema, nitatii.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipotuma kumwita Simei, akamwambia: Je? Sikukuapisha na kumtaja Bwana na kukushuhudia kwamba: Siku, utakapotoka na kwenda huko au huko, ujue kabisa, ya kuwa utakufa papo hapo? Nawe hukuniambia: Neno hili ni jema, nimesikia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa BWANA, na kukushuhudia, kusema, Siku ile ya kutoka kwako ukienda mahali po pote, ujue hakika ya kwamba kufa utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
alimwita Simei na kumwambia: “Si wewe ndiwe uliniapia kwa jina la Yawe kwamba hautatoka Yerusalema? Nami si nilikuonya kwamba hakika utakufa kama ukisubutu kwenda inje? Nawe ulikubali, ukaniambia: ‘Ni vizuri, nitatii’.