1 Kings 20:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ben-hadadi mfalme wa Aramu, alikusanya jeshi lake lote; aliungwa mkono na wafalme wengine thelathini na wawili pamoja na farasi na magari yao ya kukokotwa. Aliuendea mji wa Samaria akauzingira na kuushambulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote. Akifuatana na wafalme thelathini na wawili wakiwa na farasi na magari ya vita, akakwea kuuzingira Samaria na kuishambulia kwa jeshi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ben-hadadi mfalme wa Aramu, alikusanya jeshi lake lote; aliungwa mkono na wafalme wengine thelathini na wawili pamoja na farasi na magari yao ya kukokotwa. Aliuendea mji wa Samaria akauzingira na kuushambulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huu, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote. Akifuatana na wafalme thelathini na wawili wakiwa na farasi na magari ya vita, akakwea kuuzingira kwa jeshi Samaria na kuishambulia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huu, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote. Akifuatana na wafalme thelathini na wawili wakiwa na farasi na magari ya vita, akakwea kuuzingira kwa jeshi Samaria na kuishambulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, Ben-hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ben-hadadi mfalme wa Aramu, alikusanya jeshi lake lote; aliungwa mkono na wafalme wengine thelathini na wawili pamoja na farasi na magari yao ya kukokotwa. Aliuendea mji wa Samaria akauzingira na kuushambulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Benihadadi, mfalme wa Ushami, akavikusanya vikosi vyake vyote, hata wafalme 32 walikuwa naye pamoja na farasi na magari, akaja kuusonga Samaria kwa kuuzinga, apigane nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Beni-Hadadi mufalme wa Aramu alikusanya waaskari wake wote. Aliungwa mukono na wafalme wengine makumi tatu na wawili pamoja na farasi na magari yao ya vita. Aliuendea muji wa Samaria akauzunguka na kuushambulia.