1 Kings 20:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ben-hadadi alipokea ujumbe huu wa Ahabu wakati yeye na wafalme waliomwunga mkono walipokuwa mahemani mwao wanakunywa. Basi, akayaweka majeshi yake katika hali ya tahadhari, kuushambulia mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ben-Hadadi alisikia ujumbe huu wakati yeye na wafalme walikuwa wakinywa katika mahema yao, akawaamuru watu wake, “Jiandaeni kushambulia.” Kwa hiyo wakajiandaa kushambulia mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ben-hadadi alipokea ujumbe huu wa Ahabu wakati yeye na wafalme waliomwunga mkono walipokuwa mahemani mwao wanakunywa. Basi, akayaweka majeshi yake katika hali ya tahadhari, kuushambulia mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ben-Hadadi alisikia ujumbe huu wakati ambapo yeye na wafalme walikuwa wanakunywa katika mahema yao, na akawaamuru watu wake, “Jiandaeni kushambulia.” Kwa hiyo wakajiandaa kuushambulia mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ben-Hadadi alisikia ujumbe huu wakati ambapo yeye na wafalme walikuwa wanakunywa katika mahema yao, na akawaamuru watu wake, “Jiandaeni kushambulia.” Kwa hiyo wakajiandaa kuushambulia mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ben-hadadi alipokea ujumbe huu wa Ahabu wakati yeye na wafalme waliomwunga mkono walipokuwa mahemani mwao wanakunywa. Basi, akayaweka majeshi yake katika hali ya tahadhari, kuushambulia mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipolisikia neno hili, alikuwa akinywa na wafalme wenziwe mabandani, akawaambia watumishi wake: Haya! Jipangeni! Wakajipanga, waujie huo mji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Beni-Hadadi alipokea ujumbe huu wa Ahabu wakati yeye na wafalme waliomwunga mukono walipokuwa ndani ya mahema yao wakikunywa. Basi, akaweka waaskari wake tayari kwa kuushambulia muji ule.