1 Kings 20:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Ahabu akauliza, “Kwa msaada wa nani?” Nabii akasema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa msaada wa vijana wanaotumikia jeshi chini ya wakuu wa wilaya.’” Naye mfalme akauliza, “Ni nani atakayeanza kupigana?” Nabii akajibu, “Wewe!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahabu akauliza, “Ni nani atakayefanya hili?” Nabii akamjibu, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Maafisa vijana majemadari wa majimbo watafanya hili.’ ” Akauliza, “Ni nani atakayeanzisha vita?” Nabii akamjibu, “Ni wewe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ahabu akanena, Kwa nani? Akasema, Bwana asema hivi, Kwa vijana wa maliwali wa majimbo. Ndipo akanena, Ni nani atakayepanga vita? Naye akajibu, Ni wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Ahabu akauliza, “Kwa msaada wa nani?” Nabii akasema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa msaada wa vijana wanaotumikia jeshi chini ya wakuu wa wilaya.’” Naye mfalme akauliza, “Ni nani atakayeanza kupigana?” Nabii akajibu, “Wewe!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ahabu akauliza, “Ni nani atakayefanya hili?” Nabii akamjibu, “Hivi ndivyo asemavyo BWANA: ‘Maafisa vijana majemadari wa majimbo watafanya hili.’ ” Akauliza, “Ni nani atakayeanzisha vita?” Nabii akamjibu, “Ni wewe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ahabu akauliza, “Ni nani atakayefanya hili?” Nabii akamjibu, “Hivi ndivyo asemavyo bwana: ‘Maafisa vijana majemadari wa majimbo watafanya hili.’ ” Akauliza, “Ni nani atakayeanzisha vita?” Nabii akamjibu, “Ni wewe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ahabu akanena, Kwa nani? Akasema, BWANA asema hivi, Kwa vijana wa watawala wa majimbo. Ndipo akanena, Ni nani atakayepanga vita? Naye akajibu, Ni wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Ahabu akauliza, “Kwa msaada wa nani?” Nabii akasema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa msaada wa vijana wanaotumikia jeshi chini ya wakuu wa wilaya.’” Naye mfalme akauliza, “Ni nani atakayeanza kupigana?” Nabii akajibu, “Wewe!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahabu akauliza: Kwa msaada wa nani? Akasema: Hivi ndivyo, Bwana anvyosema: Kwa msaada wa vijana wa wakuu wa majimbo. Akauliza tena: Ni nani atakayeanza kupigana? akajibu: Wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ahabu akanena, Kwa nani? Akasema, BWANA asema hivi, Kwa vijana wa maliwali wa majimbo. Ndipo akanena, Ni nani atakayepanga vita? Naye akajibu, Ni wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Ahabu akauliza: “Kwa musaada wa nani?” Nabii akasema: “Yawe anasema hivi: ‘Kwa musaada wa vijana wanaotumikia jeshi chini ya maliwali wa majimbo.’ ” Naye mufalme akauliza: “Ni nani atakayeanza kupigana?” Nabii akajibu: “Wewe!”