1 Kings 20:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo, mtu mmoja wa Mungu akamkaribia mfalme wa Israeli, akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa kuwa Waaramu wamesema kwamba mimi Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa milimani wala si Mungu wa nchi tambarare, nitakupa ushindi dhidi ya jeshi hili kubwa, nawe utatambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mtu wa Mungu akaja na kumwambia mfalme wa Israeli, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Kwa sababu Waaramu wanafikiri Mwenyezi Mungu ni Mungu wa vilimani na sio Mungu wa mabondeni, nitalitia jeshi hili kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, Bwana asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, Bwana ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo, mtu mmoja wa Mungu akamkaribia mfalme wa Israeli, akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa kuwa Waaramu wamesema kwamba mimi Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa milimani wala si Mungu wa nchi tambarare, nitakupa ushindi dhidi ya jeshi hili kubwa, nawe utatambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu wa Mungu akaja na kumwambia mfalme wa Israeli, “Hivi ndivyo BWANA asemavyo: ‘Kwa sababu Waaramu wanafikiri BWANA ni Mungu wa vilimani na sio Mungu wa mabondeni, nitatia jeshi hili kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ndimi BWANA.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu wa Mungu akaja na kumwambia mfalme wa Israeli, “Hivi ndivyo bwana asemavyo: ‘Kwa sababu Waaramu wanafikiri bwana ni Mungu wa vilimani na sio Mungu wa mabondeni, nitatia jeshi hili kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ndimi bwana.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, BWANA asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, BWANA ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo, mtu mmoja wa Mungu akamkaribia mfalme wa Israeli, akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa kuwa Waaramu wamesema kwamba mimi Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa milimani wala si Mungu wa nchi tambarare, nitakupa ushindi dhidi ya jeshi hili kubwa, nawe utatambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, yule mtu wa Mungu alipofika kwake mfalme wa Waisiraeli, akasema: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa kuwa Washami wamesema: Bwana ni Mungu wa milima, lakini siye Mungu wa mabonde, basi, huu mtutumo mkubwa wote wa watu nitautia mkononi mwako, mpate kujua, ya kuwa mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, BWANA asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, BWANA ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, mutu mumoja wa Mungu akamukaribia mufalme wa Israeli, akamwambia: “Yawe anasema hivi: ‘Kwa sababu Waaramu wamesema kwamba mimi Yawe ni Mungu wa milima wala si Mungu wa inchi ya bonde, nitakupa ushindi juu ya kundi hili kubwa, nawe utatambua kwamba mimi ni Yawe.’ ”