1 Kings 20:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliosalia, walikimbilia mjini Afeka. Huko, kuta za mji ziliwaangukia na kuwaua watu 27,000 waliobakia. Ben-hadadi pia alikimbia na kujificha katika chumba fulani cha ndani, mjini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliobaki walikimbilia mji wa Afeki ambako elfu ishirini na saba kati yao waliangukiwa na ukuta. Naye Ben-Hadadi alikimbilia mjini na kujificha kwenye chumba cha ndani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu ishirini na saba elfu waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliosalia, walikimbilia mjini Afeka. Huko, kuta za mji ziliwaangukia na kuwaua watu 27,000 waliobakia. Ben-hadadi pia alikimbia na kujificha katika chumba fulani cha ndani, mjini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliobaki wakatorokea katika mji wa Afeki, mahali ambapo watu 27,000 waliangukiwa na ukuta. Naye Ben-Hadadi akakimbilia mjini na kujificha kwenye chumba cha ndani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliobaki wakatorokea katika mji wa Afeki, mahali ambapo watu 27,000 waliangukiwa na ukuta. Naye Ben-Hadadi akakimbilia mjini na kujificha kwenye chumba cha ndani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu elfu ishirini na saba waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliosalia, walikimbilia mjini Afeka. Huko, kuta za mji ziliwaangukia na kuwaua watu 27,000 waliobakia. Ben-hadadi pia alikimbia na kujificha katika chumba fulani cha ndani, mjini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waliosalia wakaukimbilia mji wa Afeki, boma la mji likawaangukia wale watu 27000 waliokuwa wamesalia, naye Benihadadi aliukimbilia huo mji na kuingia chumba kwa chumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu ishirini na saba elfu waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliobaki, walikimbilia katika muji wa Afeki. Kule, kuta za muji ziliwaangukia na kuwaua watu elfu makumi mbili na saba waliobakia. Beni-Hadadi vilevile alikimbia na kujificha katika chumba fulani cha ndani, katika muji.