1 Kings 20:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Ben-hadadi akamwambia, “Miji yote ambayo baba yangu alimnyanganya baba yako, nitakurudishia. Unaweza kuanzisha masoko huko Damasko kama alivyofanya baba yangu huko Samaria.” Ahabu akajibu, “Nitakuachilia kwa masharti hayo.” Hapo, akafanya mkataba naye na kumwacha huru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nitairudisha miji ambayo baba yangu aliiteka kutoka kwa baba yako. Nawe utaweka mitaa yako katika Dameski, kama baba yangu alivyofanya kule Samaria.” Ahabu akasema, “Kwa makubaliano, nitakuacha huru.” Hivyo, akaweka mkataba naye, kisha akamruhusu aende zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Ben-hadadi akamwambia, Miji ile baba yangu aliyomnyang'anya baba yako nitairudisha; nawe utajifanyia njia huko Dameski, kama baba yangu aliyoifanya huko Samaria. Ahabu akasema, Nami nitakuacha kwa mapatano haya. Akafanya mapatano naye, akamwacha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Ben-hadadi akamwambia, “Miji yote ambayo baba yangu alimnyang'anya baba yako, nitakurudishia. Unaweza kuanzisha masoko huko Damasko kama alivyofanya baba yangu huko Samaria.” Ahabu akajibu, “Nitakuachilia kwa masharti hayo.” Hapo, akafanya mkataba naye na kumwacha huru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nitairudisha ile miji ambayo baba yangu aliiteka kutoka kwa baba yako. Unaweza kuweka maeneo yako ya soko katika Dameski, kama baba yangu alivyofanya huko Samaria.” Ahabu akasema, “Katika misingi ya mkataba, nitakuachilia huru.” Kwa hiyo akaweka mkataba naye, akamruhusu aende zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nitairudisha ile miji ambayo baba yangu aliiteka kutoka kwa baba yako. Unaweza kuweka maeneo yako ya soko katika Dameski, kama baba yangu alivyofanya huko Samaria.” Ahabu akasema, “Katika misingi ya mkataba, nitakuachilia huru.” Kwa hiyo akaweka mkataba naye, akamruhusu aende zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Ben-hadadi akamwambia, Miji ile baba yangu aliyomnyang'anya baba yako nitairudisha; nawe utajifanyia njia huko Dameski, kama baba yangu aliyoifanya huko Samaria. Ahabu akasema, Nami nitakuacha kwa mapatano haya. Akafanya mapatano naye, akamwacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Ben-hadadi akamwambia, “Miji yote ambayo baba yangu alimnyanganya baba yako, nitakurudishia. Unaweza kuanzisha masoko huko Damasko kama alivyofanya baba yangu huko Samaria.” Ahabu akajibu, “Nitakuachilia kwa masharti hayo.” Hapo, akafanya mkataba naye na kumwacha huru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Benihadadi akamwambia: Miji, baba yangu aliyoichukua kwa baba yako, nairudisha; tena utajipatia njia za kuingia Damasko, kama baba yangu alivyojipatia njia ya kuingia Samaria. (Ahabu akasema): Kwa agano hili nitakuacha, ujiendee. Basi, akafanya agano naye, kisha akamwacha, ajiendee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Ben-hadadi akamwambia, Miji ile baba yangu aliyomnyang’anya baba yako nitairudisha; nawe utajifanyia njia huko Dameski, kama baba yangu aliyoifanya huko Samaria. Ahabu akasema, Nami nitakuacha kwa mapatano haya. Akafanya mapatano naye, akamwacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Beni-Hadadi akamwambia: “Miji yote ambayo baba yangu alimunyanganya baba yako, nitakurudishia. Unaweza kuanzisha masoko kule Damasiki kama vile baba yangu alivyofanya kule Samaria.” Ahabu akajibu: “Nitakuachilia kwa masharti hayo.” Hapo, akafanya mapatano naye na kumwacha huru.