1 Kings 20:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme alipokuwa anapita, nabii akamlilia akisema, “Bwana, mimi mtumishi wako nilikuwa mstari wa mbele vitani; akaja askari mmoja, akaniletea mateka mmoja na kuniambia, ‘Mlinde mtu huyu; akitoroka utalipa kwa maisha yako wewe binafsi, au kwa vipande 3,000 vya fedha.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme alipopita pale, yule nabii akamwita, “Mtumishi wako alienda vitani mahali vilikuwa kali. Mtu mmoja akanijia akiwa na mateka, akasema, ‘Mlinde mtu huyu. Akitoroka, itakuwa uhai wako kwa uhai wake, ama utalipa talanta ya fedha.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa mfalme alipopita, alimwita mfalme; akasema, Mtumwa wako aliingia katikati ya pigano; na tazama, mtu mmoja akanigeukia akaniletea mtu, akaniambia, Umlinde mtu huyu; akipotea kwa njia yo yote, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, au utatoa talanta ya fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme alipokuwa anapita, nabii akamlilia akisema, “Bwana, mimi mtumishi wako nilikuwa mstari wa mbele vitani; akaja askari mmoja, akaniletea mateka mmoja na kuniambia, ‘Mlinde mtu huyu; akitoroka utalipa kwa maisha yako wewe binafsi, au kwa vipande 3,000 vya fedha.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme alipopita pale, yule nabii akamwita, “Mtumishi wako alikwenda vitani wakati vita vilipopamba moto, mtu mmoja akanijia na mateka akasema, ‘Mlinde mtu huyu. Kama akitoroka itakuwa uhai wako kwa uhai wake, ama vipande 3,000 vya fedha.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme alipopita pale, yule nabii akamwita, “Mtumishi wako alikwenda vitani wakati vita vilipopamba moto, mtu mmoja akanijia na mateka akasema, ‘Mlinde mtu huyu. Kama akitoroka itakuwa uhai wako kwa uhai wake, ama vipande 3,000 vya fedha.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa mfalme alipopita, alimwita mfalme; akasema, Mtumwa wako aliingia katikati ya pigano; na tazama, mtu mmoja akanigeukia akaniletea mtu, akaniambia, Umlinde mtu huyu; akipotea kwa njia yoyote, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, au utatoa talanta ya fedha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme alipokuwa anapita, nabii akamlilia akisema, “Bwana, mimi mtumishi wako nilikuwa mstari wa mbele vitani; akaja askari mmoja, akaniletea mateka mmoja na kuniambia, ‘Mlinde mtu huyu; akitoroka utalipa kwa maisha yako wewe binafsi, au kwa vipande 3,000 vya fedha.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, mfalme alipopita, yeye akamlilia mfalme akisema: Mtumishi wako alikuwa amekwenda penye yale mapigano; mara mwenzangu aliyekuwa ameondoka akaniletea mtu, akaniambia: Mwangalie mtu huyu! Atakapopotea, mwenyewe utaingia mahali pake au utajikomboa kwa kulipa kipande cha fedha, ndio shilingi 12000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa mfalme alipopita, alimwita mfalme; akasema, Mtumwa wako aliingia katikati ya pigano; na tazama, mtu mmoja akanigeukia akaniletea mtu, akaniambia, Umlinde mtu huyu; akipotea kwa njia yo yote, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, au utatoa talanta ya fedha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme alipokuwa anapita, nabii akamulilia akisema: “Bwana, mimi mutumishi wako nilikuwa kwa mustari wa mbele katika vita. Kukakuja askari mumoja, akaniletea mateka mumoja na kuniambia: ‘Umulinde mutu huyu. Akitoroka utalipa kwa maisha yako wewe peke yako, au kwa bei ya vikoroti elfu tatu vya feza.’