1 Kings 21:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, tafuteni walaghai wawili wamkabili na kumshtaki wakisema: ‘Wewe umemwapiza Mungu na mfalme.’ Kisha mtoeni nje, mkamuue kwa kumpiga mawe!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waketisheni walaghai wawili mkabala naye, nao washuhudie dhidi yake kuwa amemlaani Mungu na mfalme pia. Kisha mtoeni nje na kumpiga kwa mawe hadi afe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, tafuteni walaghai wawili wamkabili na kumshtaki wakisema: ‘Wewe umemwapiza Mungu na mfalme.’ Kisha mtoeni nje, mkamuue kwa kumpiga mawe!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ketisheni watu wawili wabaya kabisa mkabala naye, nao washuhudie kuwa yeye amemlaani Mungu na mfalme. Kisha mtoeni nje na kumpiga kwa mawe hadi afe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini waketisheni watu wawili wabaya kabisa mkabala naye, nao washuhudie kuwa yeye amemlaani Mungu na mfalme. Kisha mtoeni nje na kumpiga kwa mawe hadi afe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkawaketishe watu wawili, watu walaghai, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, tafuteni walaghai wawili wamkabili na kumshtaki wakisema: ‘Wewe umemwapiza Mungu na mfalme.’ Kisha mtoeni nje, mkamuue kwa kumpiga mawe!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wekeni kila kando yake watu wawili wasiofaa, wapate kumsingizia kwamba: Amemtukana Mungu na mfalme. Kisha mtoeni mjini, mmpige mawe, afe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, mutafute watenda maovu wawili wapate kumushuhudia na kumushitaki wakisema: ‘Wewe umemutukana Mungu na mufalme.’ Kisha mumupeleke inje, mumwue kwa kumutupia mawe!”