1 Kings 21:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale walaghai wawili wakaketi kumkabili Nabothi, kisha wakamshtaki hadharani wakisema, “Nabothi amemwapiza Mungu na mfalme.” Basi, Nabothi akatolewa nje ya mji, akauawa kwa kupigwa mawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha walaghai wawili wakaja wakaketi mkabala naye; nao wakaleta mashtaka dhidi ya Nabothi mbele ya watu, wakisema, “Nabothi amemlaani Mungu na mfalme pia.” Kwa hiyo wakamtoa nje na kumpiga kwa mawe hadi akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale walaghai wawili wakaketi kumkabili Nabothi, kisha wakamshtaki hadharani wakisema, “Nabothi amemwapiza Mungu na mfalme.” Basi, Nabothi akatolewa nje ya mji, akauawa kwa kupigwa mawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wawili wabaya kabisa wakaja wakaketi mkabala naye, nao wakaleta mashtaka dhidi ya Nabothi mbele ya watu, wakisema, “Nabothi amemlaani Mungu na mfalme.” Kwa hiyo wakamtoa nje na kumpiga kwa mawe hadi akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wawili wabaya kabisa wakaja wakaketi mkabala naye, nao wakaleta mashtaka dhidi ya Nabothi mbele ya watu, wakisema, “Nabothi amemlaani Mungu na mfalme.” Kwa hiyo wakamtoa nje na kumpiga kwa mawe hadi akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale walaghai wawili wakaketi kumkabili Nabothi, kisha wakamshtaki hadharani wakisema, “Nabothi amemwapiza Mungu na mfalme.” Basi, Nabothi akatolewa nje ya mji, akauawa kwa kupigwa mawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaja watu wawili wasiofaa kitu, wakakaa kando yake, kisha hao watu wasiofaa kitu wakamsingizia Naboti mbele ya watu kwamba: Naboti amemtukana Mungu na mfalme; kwa hiyo wakamtoa nje ya mji, wakampiga mawe, mpaka akifa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watenda maovu wawili wakaikaa kwa kumushuhudia Naboti, kisha wakamushitaki mbele ya watu wote wakisema: “Naboti amemutukana Mungu na mufalme.” Basi, Naboti akapelekwa inje ya muji, akauawa kwa kutupiwa mawe.