1 Kings 21:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwambie, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Umeua na kumiliki pia?’ Mwambie Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, ndipo watakapoilamba damu yako.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Je, hujamuua mtu na kuitwaa mali yake?’ Kisha umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Mahali mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba damu yako pia; naam, yako wewe!’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukamwambie, ukisema, Bwana asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, Bwana asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwambie, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Umeua na kumiliki pia?’ Mwambie Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, ndipo watakapoilamba damu yako.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umwambie, ‘Hivi ndivyo BWANA asemavyo: Je, hujamwua mtu na kuitwaa mali yake?’ Kisha umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo BWANA: Mahali ambapo mbwa walilamba damu ya Nabothi, mbwa watailamba damu yako, naam, yako wewe!’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umwambie, ‘Hivi ndivyo bwana asemavyo: Je, hujamuua mtu na kuitwaa mali yake?’ Kisha umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo bwana: Mahali ambapo mbwa waliramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba damu yako, naam, yako wewe!’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwambie, Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Umeua na kumiliki pia?’ Mwambie Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, ndipo watakapoilamba damu yako.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umwambie kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kumbe umeua, kisha ukazitwaa mali za mfu? Kisha umwambie kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mahali pale, mbwa walipoilamba damu ya Naboti, palepale mbwa watailamba nayo damu yako wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umwambie, Yawe anasema hivi: ‘Umeua na kutwaa mali yake vilevile?’ Umwambie Yawe anasema hivi: ‘Pahali pale imbwa walipoilambulia damu ya Naboti, ndipo watakapoilambulia damu yako.’ ”